Ukiachana na upinzani mkali wa vilabu vya Azam, Simba na Yanga kwenye soka la Bongo, wachezaji wa vilabu hivyo ni washkaji sana wanapokuwa nje ya uwanja.
Jana wakati pambao la Azam Sports Federation Cup linaendelea kati ya Azam FC dhidi ya Africa Lyon, wacheaji wa kigeni wanaofanya vizuri kwenye ligi ya Vodacom Tanzania bara walikutana na kupiga story kwa muda mrefu kitu ambacho kiliwavutia mashabiki na wapenzi wengi wa soka waliokuwa wakishuhudia mchezo huo.
Golikipa wa Simba Vicent Agban, beki kisiki wa Azam FC Pascal Wawa pamoja na beki wa Yanga Vicent Bossou walionekana wakifurahi pamoja mbali ya timu zao kuwa na upinzani mkali hasa kwenye ligi ya Vodocom Tanzania bara katika kuwania ubingwa wa ligi hiyo.
Kwenye mchezo wa Mapinduzi Cup kati ya Yanga dhidi ya Azam ziliibuka vurugu mara kadhaa baina ya wachezaji na kupelekea Jonh Bocco kutolewa uwanjani kwa kadi nyekundu.
Lakini vurugu ambazo ziliusimamisha mchezo huo kwa muda mrefu ilikuwa ni kati ya Wawa na Ngoma. Bossou alijitahidi kuwasuluhisha wawili hao hadi wakaelewana na kurejea kwenye hali ya kawaida.
0 comments:
Post a Comment