Leo katika pitapita za hapa na pale camera ya simbadume.co.tz ‘Timu ya Ushindi’ imefanikiwa kudaka picha za Star wa Simba SC na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Ibrahim Aib akiwa ndani ya gari yake maeneo ya uwanja wa Karume.
Ajib alikuwepo kwenye uwanja wa Karume kushuhudia pambano la Azam Sports Federation Cup kati ya Africa Lyon dhidi ya Azam FC mchezo uliomalizika kwa Azam kupata ushindi wa magoli 4-0.
Baada ya mchezo huo kumalizika Ajib aliekea alikoegesha ndinga yake na kuchomoka akiwa na baadhi ya watu wake wa karibu ambao aliambatana nao kushuhudia game hiyo.
0 comments:
Post a Comment