Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitatangaza timu iliyopanda Ligi Kuu
msimu ujao kutoka Kundi C, mpaka itakapoamuliwa na vyombo husika vya
TFF baada ya michezo ya kundi hilo kuchezwa leo jioni katika viwanja
tofauti nchini.
TFF
imefikia hatua hiyo ili kupata nafasi ya kupitia taarifa za michezo
kati ya JKT Kanembwa v Geita Gold na Polisi Tabora v JKT Oljoro
iliyochezwa jana jioni katika mikoa ya Kigoma na Tabora.
Taarifa za michezo hiyo kutoka kwa wasimamizi husika na vyanzo vingine vinakusanywa ili zifanyiwe kazi na vyombo husika vya TFF.
Katika
michezo hiyo ya leo, Geita iliibuka na ushindi wa mbao 8 – 0 dhidi ya
JKT Kanembwa, huku Polisi Tabora wakiibuka na ushindi wa mabao 7 – 0
dhidi ya JKT Oljoro.
0 comments:
Post a Comment