Uvumilivu umemshinda Mohhamed Dewji baada ya mwendelezo wa matokeo mabovu ya klabu ya Simba ambayo imemaliza ligi kwa kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Ruvu JKT na kushindwa kumaliza ligi nyuma ya wapinzani wa Yanga ambao ni mabingwa wa VPL kwa mara ya pili mfululizo.
Kutokana na Simba kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya msimu huu, VPL pamoja na Azam Sports Federation Cup (FA Cup) MO ambaye ni bilionea wa kitanzania aliyewahi kuomba kuinunua ya Simba ameamua kufikisha ujumbe kwa klabu hiyo ni namna gani anaguswa na matokeo mabaya ya klabu hiyo.
MO ameandika ujumbe kwenye account yake ya twitter unaosomeka hivi: “Simba mnatunyima raha, tumechoka kutaniwa na kutukanwa mitaani”.
Simba imekuwa na matokeo mabaya katika mechi zake za mwishoni mwa msimu huu baada ya kukubali vipigo mfululizo kutoka kwa Toto Africans, Mwadui FC na JKT Ruvu huku wakiambulia sare pekee dhidi ya Azam katika mechi zao nne za mwisho.
Licha ya tajiri huyo wa kitanzania kuomba auziwe asilimia 51 ya hisa za Simba ili kwa zaidi ya kitita cha bilioni 20 za kitanzania, bado uongozi wa klabu hiyo umekuwa ukisuasua kumkabidhi timu MO ambaye lengo lake ni kuiendesha Simba kama kampuni.
0 comments:
Post a Comment