Klabu ya soka ya Simba August 13 imekamilisha ahadi yake ya kugawa mipira kwa shule za msingi, mwisho wa wiki iliyopita Simba ilipanga ratiba ya kutembelea shule tatu za msingi.
Simba imetembelea shule ya Msingi Ndugumbi iliyopo Magomeni Mwembechai.
Rais wa Simba Evans Aveva akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG Group, Imani Kajula wamekabidhi mipira kwa shule nyingine mbili ambazo awali walishindwa kuzitembelea kutokana na kukosa muda, Shule zilizopewa mipira August 13 ni Shule yaMsingi Mikocheni na Shule ya Msingi Chang’ombe.
Nimekusogezea Picha za tukio lote zawadi zilivyokabidhiwa Shule za Msingi.
0 comments:
Post a Comment