Baada ya
kukiangalia kikosi chake kwa umakini katika michezo sita iliyopita ya kirafiki,
Kocha Mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, amesema kuwa, sasa kikosi chake
kinakabiliwa na tatizo moja la mshambuliaji pekee ambalo yupo mbioni kulitatua
kabla ya kuanza kwa ligi kuu.
Mpaka sasa,
kikosi cha Kerr kinaundwa na washambuliaji watatu tu wa kati ambao ni Mussa
Hassan Mgosi, Ibrahim Ajibu pamoja na Mganda, Hamis Kiiza aliyejiunga hivi karibuni,
huku Elias Maguli akiwekwa pembeni.
Kerr amesema kuwa, mpaka sasa mawazo yake yote anayaelekeza katika
kuwania saini ya mshambuliaji ambaye atakuja kuungana na wachezaji waliopo sasa
kwa ajili ya kujiwinda na msimu ujao.
“Kwa sasa tupo
katika harakati za kuwinda saini ya mshambuliaji wa kati ambaye atakuja
kuongeza nguvu katika kikosi chetu, ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao.
“Naamini kama tukifanikiwa kupata saini ya mshambuliaji huyo, itakuwa ndiyo mwisho wa kufanya usajili kwa sasa ndani ya timu yetu na ninaamini tutakuwa tayari kwa ajili ya kuanza harakati za kupigania ubingwa,” alisema Kerr.
0 comments:
Post a Comment