Na Mwandishi wetu, Tanga
Uongozi wa klabu ya African Sports ya jijini Tanga leo umeamuwa kuvunja mkataba na kocha wao Ramadhani Aluko.
Uongozi wa klabu ya African Sports ya jijini Tanga leo umeamuwa kuvunja mkataba na kocha wao Ramadhani Aluko.
Akizungumza nami mchana wa leo mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu
hiyo Anton Kimath amesema wameamuwa kuchukuwa uamuzi huo kutokana na
timu yao kuwa na matokeo mabovu.
Kimath alisema kuwa wanamshukuru Aluko kwa kuweza kuisaidia timu yao
kupata point 20 mpaka sasa lakini ameshindwa kufikia lengo la kuinusuru
timu kushuka daraja.
Kwa upande wake kocha huyo amesema viongozi wa timu hiyo wamemtoa
kafara kwani ndani ya timu hiyo kuna matatizo mengi sana yanayowakabili
wachezaji kama wachezaji kukosa stahiki zao kwa wakati wachezaji kukosa
huduma za kiafya.
Aluko amesema kuwa kikosi cha timu hiyo kimesajiliwa kimakundi kila
kiongozi akiwa na wachezaji wake hali inayomuwia vigumu kupanga timu
kwani kila upande ukitaka wacghezaji wake ndio wapewe nafasi.
Aluko aliikuta nAfrican Sports wakiwa na point 3 baada ya kucheza
michezo 8 wakifungwa 7 na kushinda chezo 1 chini ya uongozi wake
amekiongoza kikoisi cha timu hiyo kwa michezo 15 akishinda michezo 4
sare 4 akifungwa 6 anaondoka African Sports akiwaachia point 20.
Tatizo kubwa ndani ya timu hiyo ni makamu mwenyekiti Abdul Ahmed
Bosnia ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa wadau wengi kujiweka pambeni
ya timu hiyo wadau ambao wameamua kujiweka kando ni kama Mohamed Salim
amkurugenzi wa kampuni ya RATCO, wengine ni mchezaji wa zamani wa timu
hiyo Salim Wazir, mwenyekiti wa timu hiyo aliyejiuzulu ambaye ametumia
kiasi cha shilingi milioni 250 kuipandisha timu kutoka daraja la nne
mpaka ligi kuu Hassan Kessy Hariche.
Wote hao wameamuwa kujiweka kando kutokana na majungu na fitna za
kiongozi huyu ambasye kwa hakika amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani
ametengeneza wanachama wengi wanaomlinda na kumtetea kwa nguvu zote.
0 comments:
Post a Comment