Anga
ya michezo hasa ule wa soka kwa Afrika Mashariki umepata msiba mkubwa
baada ya kipa Abel Dhaira, kufariki dunia nchini Iceland alikokuwa
anasumbuliwa na kansa ya utumbo.
Dhaira
amefariki jana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema amepokea kwa
mshituko mkubwa kifo cha kipa huyo wa zamani wa Simba ya Tanzania, URA,
Express na timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.
Aidha,
Museveni amesema serikali yake itagharimia kila kitu ikiwemo
kuusafirisha mwili wake pamoja na mazishi, huku akiwapa pole wanafamilia
wa Dhaira na familia yote ya wapenda michezo katika kipindi hiki cha
majonzi.
0 comments:
Post a Comment