1) Hadhira/mashabiki na wachezaji lazima wafurahie kuangalia na kucheza soka. Soka ni mchezo wa kuvutia kwa watazamaji na wachezaji, kama sio wa kuvutia basi mchezo huo sio soka.
2) Mbinu na kuziwezesha mbinu hizo kufanya kazi dimbani ndio jukumu hasa la mchezaji.
3) Mara zote inabidi uwe na utayari wa kutaka kujifunza vitu vipya kutoka kwa wengine.
4) Furaha ni jambo la msingi kwenye maisha, lakini inahitajika hasa kwenye mchezo wa soka.
5) Heshima Kwa wengine – wachezaji wenzako, mashabiki/jamii, refa, nk, ni jambo la msingi katika michezo na maisha kiujumla.
6) Inabidi ukubaliane na ukweli kwamba wengine watafanya makosa na inabidi kuwasaidia kuyarekebisha aidha kwenye maisha ya kawaida na hata uwanjani, na wao pia watatusaidia tutakapohitaji msaada.
7) Kwenye soka na maisha kiujumla ni muhimu kujua namna na ya kufanya kazi na wenzako kama timu, kuelewa kwamba mchezaji mmoja pekee hawezi kushinda mechi.
8) Kujitoa na kufanikisha kwa asilimia 100 ni lazima kwa asilimia zote kwenye soka.
9) Mwanasoka ana majukumu makubwa katika jamii. Ni mfano wa kuigwa kwa watu wengi na anawakilisha kundi kubwa la mashabiki zake.
10) Soka ni shule nzuri ya maendeleo binafsi na inasaidia ukuaji wa kifikra wa mtu.
0 comments:
Post a Comment