Mbunge anayepambana kulichukua Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia amejikuta katika wakati mgumu sasa kutokana na mgombea Exaud Makyao kutangaza nia ya kugombea jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Akitangaza nia yake ya kulinyakua Jimbo hilo linalozozaniwa na wababe wawili wenye historia tofauti katika medani ya siasa hapa nchini, katika mkutano wa kampeni kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa katika kijiji cha Holili wilayani Rombo mkoani hapa, Makyao aliweka bayana kuwa ana ubavu wa kupambana na Mbatia.
Makyao aliongeza kusema kwamba ujio wa Mbatia katika Jimbo la Vunjo kumeibua maswali mengi kutokana na kwamba wakazi wa jimbo hilo hupiga kura ya ndio kwa mgombea ambaye wanamfahamu kwa muda mrefu.
“Mbatia haeleweki alikotokea, ndio changamoto kubwa hapo la sivyo licha ya muungano wetu katika UKAWA tusipokuwa makini jimbo hilo tunaweza tusilipate na likarudi kwa mwenyewe (Mrema).” alisema mgombea huyo.
Mgombea huyo alisema wakati mwingine umaarufu wa chama unaweza kukupa ulaji na ikawa mteremko kuelekea uchaguzi kama ilivyo kwa baadhi ya wagombea ambao vyama vyao vinawabeba lakini kumbe hawafahamika kabisa kwa kundi kubwa la wapiga kura.
Pia Makyao alisema kauli ya Mbunge wa sasa wa jimbo hilo aliyoitamka akiwa bungeni mjini Dodoma kwamba anaomba msaada wa serikali na wabunge kwenda kumuokoa asinyang’anywe mikoba imemtia hofu Agustino Lyatonga Mrema na James Mbatia hasa ikizingatiwa hata Mbatia naye alipewa ulaji wa kutinga bungeni baada ya kuonwa na Rais Jakaya Kikwete.
“ Mrema amechanganyikiwa kwa sasa kutokana na kwamba kuomba kwake msaada kwa Rais Jakaya Kikwete na baadaye JK kufanya uteuzi wa James Mbatia, kumesababisha hali ya hofu kuelekea kinyang’anyiro hicho mwaka ujao, hususani kwa Mrema ambaye anahisi kama kuna zengwe amefanyiwa.” alisema Makyao.
Hata hivyo Makyao aliweka bayana kwamba Ukawa itakutana kujadiliana wakati utakapofika nani anakubalika zaidi kuliko mwenzake ili kuweza kumsimamisha mgombea mmoja kama walivyokubaliana na kuongeza kwamba ana ubavu wa kumshusha Mbatia.
Katika mkutano huo wa kampeni kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA-Kilimanjaro) kupitia kampeni mpya inayojulikana kwa jina la “ Kampeni Delete CCM” iliyozinduliwa hivi karibuni liliwakaribisha wanachama wapya 45 walioamua kukitumia chama hicho katika kijiji cha Holili.
Aidha Mwenyekiti wa Bavicha mkoani hapa, Dickson Kibona alisema hujuma kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mkoani mwake zimeanza kujitokeza ambapo kuna baadhi ya maafisa watendaji wamekuwa wakijiingiza kukisaidia Chama cha Mapinduzi (CCM) hali ambayo ameiita kuwa itaamsha vurugu kubwa endapo haitadhibitiwa mapema.
Kibona aliongeza kusema baadhi ya maafisa watendaji wamekuwa wakiitwa katika vikao vya usiku vinavyofanywa na CCM na kuelekezwa namna watakavyoweza kuimaliza Chadema.
“Baadhi ya vijiji vilivyopo Usseri, wilayani Rombo tumepata taarifa zao kuhusu mchezo wa maafisa watendaji wa kijiji, kuvunja maadili ya kazi yao hali wakijua wao ndio wasimamizi wa uchaguzi, kibaya zaidi wengine wameanza kutishiwa endapo hawatakubali watakiona cha moto, tupo katika harakati za kupeleka kwa maandishi vitisho hivyo Polisi.”
Itakumbukwa kwamba uchaguzi wa serikali za mitaa umepangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2015.

0 comments:
Post a Comment