MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

OKWI AANZA KUPATA MATIBABU YA KIFUNDO CHA MGUU KWAO UGANDA



Kiungo nyota wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi ambaye kwa sasa yupo Uganda katika mapumziko mafupi baada ya kusimama kwa ligi, leo Jumatatu anatarajia kuanza rasmi matibabu ya maumivu ya kifundo cha mguu wake wa kulia yaliyokuwa yanayomsumbua tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu.


Okwi amesema iwapo atapona kabisa, basi anaamini makali yake yataongezeka maradufu.

Tayari amefumania nyavu mara tatu katika mechi saba, alisema ndoto zake msimu huu ni kuhakikisha Simba inafanya vizuri na kumaliza ikiwa na ubingwa wa ligi kuu (VPL), hivyo anamwomba Mungu amjalie aweze kupona mapema jeraha hilo ambalo anasema linamkosesha amani kila siku.

“Kesho (leo) ndiyo natarajia kuanza matibabu baada ya kukamilika kwa taratibu zote, hivyo namuomba Mungu anijalie nipone mapema.

“Natamani safari hii kuiona Simba inakuwa bingwa, hivyo ndoto hizo ili ziweze kutimia, inatakiwa wachezaji wote kuwa fiti. Hivyo nawaomba wapenzi na mashabiki wa timu yetu waniombee ili niweze kupona haraka,” alisema Okwi.


Uongozi wa Simba umepanga Okwi kutibiwa na daktari maalum hukohuko kwao Uganda katika kipindi hiki ambapo ligi imesimama.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment