Kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Peter Mwalyanzi atapumzika kwa siku moja.
Mapumziko hayo amepewa baada ya kuumia na kutolewa nje wakati wa mechi ya kirafiki wakati Simba ilipoivaa URA jijini Dar, jana.
Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema Mwalyanzi hakupata majeraha makubwa.
"Kweli aliumia, lakini hayakuwa majeraha makubwa. Tumempa siku moja ya mapumziko na baada ya hapo ataungana na wenzake mazoezini," alisema.
Kuumia kwa Mwalyanzi kuliwalazimisha Simba kucheza pungufu licha ya kuibuka na ushindi baadaye na hiyo ilitokana na wao kuwa wameishamaliza nafasi zao za mabadiliko.

0 comments:
Post a Comment