MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

NIMEKUBANDIKIA MAHOJIANO YA SELEMAN MATOLA NA TOVUTI YA SIMBA SC

Matola (kulia) alicheza soka siku ya Simba Day
Simbasports.co.tz  jana ilipata nafasi ya kuongea na kocha msaidizi wa Timu ya Simba, Seleman Matola kuhusu maendeleo ya timu, ushauri kwa kikosi kizima pamoja na Uongozi.
Haya ndio yalikuwa mahojiano yao na Matola:-
Simbasports.co.tz: Habari yako Matola?
Matola: Namshukuru Mungu mimi nipo salama kabisa, naendelea vizuri na kazi zangu za kila siku katika kushirikiana na kocha Dylan Kerr kuifundisha timu yetu ya Simba.
Simbasports.co.tz: Vipi unaonaje kikosi chako cha Simba katika kujiandaa na ligi kuu Tanzania Bara?
Matola: kikosi changu kipo vizuri sana tena sana, kama ambavyo unaona mpaka sasa hatujapoteza hata mechi moja ya kirafiki tangu tuanze kufanya mazoezi ya kujitayarisha na kuanza kwa ligi. Hili ni jambo kubwa na la kutia faraja sana kuona kuwa wachezaji wanafuata mafundisho tunayowapatia sisi kama makocha ili kuweza kuupata ushindi katika michezo yetu yote.
Simbasports.co.tz: Kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Simba na URA tuliona kuwa Simba ikicheza ikiwa na wachezaji 9 uwanjani na kuweza kushinda,  kwa nini mliamua kuchezesha wachezaji 9 baada ya mchezaji Peter Mwalyanzi kuumia?
Matola: Unajua kwenye mpira kuna mambo mengi sana yanaweza kutokea, mchezaji kuumia,  mchezaji kupewa kadi nyekundu hata mchezaji kuwa nje ya mchezo ni kawaida, hivyo ni lazima kuijenga timu ikijua kuwa hata wakiwa pungufu bado wanatakiwa kuwa na ari ya ushindi na ndicho kilichotokea kwenye mechi ya Jumamosi na Klabu ya URA ambapo tulipata goli la pili tukiwa tunacheza wachezaji 9.
Simbasports.co.tz: Je una ushauri gani kwa wachezaji?
Matola: Kwanza ni kuendeleza usikivu wanaouonesha kwa Makocha na Viongozi wetu wa Simba kwa ujumla, kufanya mazoezi ya kutosha pamoja na kujituma zaidi.
Simbasorts.co.tz: Una ushauri gani kwa Viongozi wa Simba?
Matola: Ushauri wangu ni uleule kila siku viongozi ni lazima wadumishe mshikamano walionao sasa hivi, ni lazima wawe na umoja na kuendelea kuwa karibu na timu yao.
Kocha msaidizi Matola amezaliwa tarehe 24 – 4 – 1978 na aliichezea Simba kwa mafanikio makubwa sana katika miaka ya 2000.
18Aug2015
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment