Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo asubuhi kimeanza mazoezi ya kujiandaa na pambano la kuwania kufuzu kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya timu ya Nigeria mchezo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 5, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kikosi kilichofanya mazoezi siku ya leo ni sehemu ndogo ya timu nzima ya Taifa kwasababu wachezaji wengi wa timu za Yanga na Azam wamezuiwa kujiunga na timu hiyo kutokana na kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii ambayo itapigwa Agosti 22 mwaka huu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu msimu wa 2015-2016.
Wachezaji ambao wapo kambini mpaka sasa ni 17 lakini awali kocha mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa alitangaza kikosi cha wachezaji 29 ambacho kilitakiwa kuingia kambini. Wachezaji wa kimatafa wao watawasili baadae kwasababu ruhusa yao kutoka kwenye vilabu vyao kwenda kwenye timu za taifa inatokana na kalenda ya FIFA.
Kutokana na Yanga pamoja na Azam kuzuia wachezaji wao wakijiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii, MKwasa amelazimika kuwaita wachezaji wengine 10 ili kujaribu kuziba nafasi za wachezaji wengine ambao bado hawajaripoti.
Wachezaji walioongezwa kwenye kikosi cha Stars ni Mohamed Yusufu (Tanzania Prisons), Sid Mohame (Mibwa Sugar), Vicent Andrew (Mtibwa Sugar), Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, (Simba SC), Ibrahim Ajibu (Simba SC), Hamisi Ally (KMKM), Juma Mbwana (KMKM), Tumba Swed (Coastal Union), Samwel Kamuntu (JKT Ruvu) na Ibrahim Hilka (Zimamoto-Zanziabar) .
0 comments:
Post a Comment