Katika kikao cha Bunge leo Novemba 21, Mbunge Peter Msigwa aliuliza swali kuhusiana na kitendo cha Mawaziri na Wabunge kutosomesha watoto wao wala kutotibiwa ndani ya Nchi; “…Tafiti zinaonesha kwamba wale watu ambao ni wataalamu hawarudi kwenye maeneo yao.. Kwa kuwa katika sekta ya elimu na afya imeonyesha kwamba viongozi kuanzia Mawaziri pamoja na Wabunge hawaamini mfumo wa elimu ndio maana hawapeleki watoto wao kwenye shule hizo za Serikali ..
“..Hata Mawaziri wenyewe hawaamioni mfumo wa afya ndio maana na wenyewe hawatibiwi kwenye Hospitali za nchini, pamoja na Wabunge. Je haoni ni wakati muafaka sasa kwa Serikali kuleta sheria ambayo italazimisha Waziri, Wabunge wanaohusiana na Sekta hizi walazimishwe kusomesha watoto wao na kutibiwa katika Hospitali hizo wanazoziongoza ili kuleta adabu na ufanisi katika utendaji kusudi wananchi watuamini kwamba Tunaongoza Sekta ambazo na sisi wenyewe tunaziamini…“– Msigwa.
Akijibu swali hilo Waziri Celina Kombani amesema; “… Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Msigwa ambalo limetoka nje ya Mada kama ifuatavyo; kiongozi ni mfano kwa hiyo Mheshimiwa Msigwa anaweza akaanza yeye kutibiwa kwenye Hospitali za kawaida, akawa ni mfano kwa wengine, basi na wengine tutafuata…“
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment