MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

Nakukutanisha na mapacha wasio na birthday moja.

twins
Mapacha wenyewe ndio hawa ambapo wote ni wa kike.
Kwa kawaida mapacha wanazaliwa siku moja wakiwa wametofautiana muda mfupi sana na mara nyingi huwa inakuwa ni sekunde au dakika toka wakati anapozaliwa mmoja mpaka wakati anakozaliwa mwingine na hii ni kwa sababu kibaiolojia haiwezekani kwa watoto wawili kutoka tumboni kwa wakati mmoja.
Lakini Uingereza imeweka rekodi hii ya kuwa na watoto mapacha ambao siku zao za kuzaliwa ziko kwenye tarehe mbili tofauti yaani kama mmoja amezaliwa tarehe 1 mwingine amezaliwa tarehe 2.
Huko Bolton watoto Scarlett na Robbyn wameweka rekodi hii baada ya mama yao kujifungua watoto wawili kwenye tarehe mbili tofauti, ilianza kama utani wakati ambapo mama huyo aliingia kwenye maumivu ya uchungu wa kuzaa saa chache kabla ya kuingia kwa siku mpya ambayo kwa mahesabu ya kidunia huanza saa sita usiku.
Hawa ni mapacha ambao mwaka 2013 walivunja rekodi ya kuzaliwa katika nchi mbili tofauti, mmoja alizaliwa England na mwingine Scotland ambapo wa pili alizaliwa dakika 100 baada ya wa kwanza kuzaliwa.
Hawa ni mapacha ambao mwaka 2013 walivunja rekodi ya kuzaliwa katika nchi mbili tofauti, mmoja alizaliwa England na mwingine Scotland ambapo wa pili alizaliwa dakika 100 baada ya wa kwanza kuzaliwa.
Kabla ya kufika kwa saa sita kamili usiku majira kama ya 5 na dakika 45 usiku mama huyo alijifungua mtoto mmoja huku akingojea kujifungua mwingine kwani alifahamu fika amebeba mapacha.
Mtoto mwingine alikuja kuzaliwa dakika 18 baada ya saa sita usiku kupita na hivyo kufanya ionekane kuwa watoto mapacha Robyn na Scarlett wamezaliwa kwenye tarehe za siku mbili tofauti mmoja akiwa amezaliwa saa tano usiku kabla ya siku mpya kuanza na mwingine akiwa amezaliwa baada ya saa sita usiku saa chache baada ya siku mpya kuanza.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment