MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

BWANA MDOGO ASHINDA URAIS CHAMA CHA SOKA KENYA


Nick Mwendwa Nick Mwendwa ameibuka mshindi kwenye kinyang’anyiro cha urais wa shirikisho la soka la nchini Kenya (Football Kenya Federation-FKF).
Mwendwa amembwaga gwiji ambaye ni rais wa klabu ya Gor Mahia Ambrose Rachier,na kushinda uchaguzi huo huku rais aliyekuwa akiondoka madarakani Sam Nyamweya akijitoa katika kinyang’anyiro hicho dakika za mwisho.
Nick Mwendwa, 37, mwenyekiti wa klabu ya Kariobangi Sharks ameshinda uchaguzi wa urais wa FKF baada ya kupata kura 50 kati ya 77 akifuatiwa na Rachier aliyepata kura 27.
Kwa matokeo hayo yamemfanya Nick Mwendwa kuwa rais mpya wa FKF na kuchukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Sammy Sholei.
Wakenya wamefurahia mabadiliko hayo na kusema kwamba imekuwa ni muda mrefu wamekuwa wakitaka mabadiliko yaje mapema lakini wanaimani na Mwendwa wakisema ataweza kuleta mabadiliko kwasababu ni kijana ambaye amekuwa na mipango mizuri.
Ukiangalia kwenye mitandao ya kijamii kama twitter na facebook watu wanasema huo utakuwa mwanzo mpya wa soka la Kenya.
Angalia baadhi ya twits za kumpongeza Nick Mwendwa baada ya kutangazwa rais mpya wa FKF.
COFEK, Kenya ‏@ConsumersKenya: Congratulations Nick Mwendwa for being elected FKF President with landslide win! Good luck #TeamCofek #FKFElections.
FERDINAND OMONDI ‏@FerdyOmondi:Nick Mwendwa was totally ahead of the pack even in his thoughts and how he argued his case. Good luck to him.
#FKFElections. Waweru. ‏@martinwilshere: Congrats to Nick Mwendwa. Kenyan football has won #FKFElections. Ole Teya ‏@Kevin_teya: Ladies and Gentlemen your new FKF President is NICK MWENDWA. Congratulations young Tuck.
#FKFELECTIONS. THE SEASON ‏@castrofy26: And yes…a dawn for soccer it is, Nick is the new FKF chairman, congratulations.#FKFElections.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment