MOROCCO |
Kocha Hemed Morocco huenda asijiunge tena na Simba baada ya suala lake kuingia figisu.
Hali hiyo inatokana na kocha huyo kuamua kutosaini mkataba kama walivyokuwa wamekubaliana baada ya kugundua mshahara wake ulikuwa umepunguzwa.
“Kweli tulikuwa tumekubaliana kila kitu, nilisafiri kutoka Zanzibar kuja hapa Dar es Salaam kwa ajili ya kumalizana na kusaini mkataba. Hii ilikuwa hivi baada ya kuwa tumeanza mazungumzo kule Zanzibar.
“Lakini ajabu nimekuja kuona mkataba umebadilishwa na kuna vipengele havipo sawa, sasa naona haitakuwa kama nilivyotarajia,” alisema.
Ingawa Morocco amekuwa akificha kuhusiana na suala hilo, lakini kipengele kilichobadilishwa ni cha mshahara na inaonekana kocha huyo msaidizi wa Taifa Stars hatakubali.
Kama itakuwa hivyo, Simba itaendelea kusaka kocha mwingine na inawezekana akawa anatokea nje ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment